Swimming NewsTAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - PRESS RELEASE.

Kikao kilichofanyika tarehe 27 mwezi Machi 2013 katika ukumbi wa Navy Beach Kigamboni juu ya maandalizi ya event ya Mv Mama.
Pili Omari - Mrs Major General  SS Omar (Tanzania Navy Commander) ambaye ni mshauri mkuu wa event ya Mv Mama alisema, ameona umuhimu wa yeye kushiriki na kuwashauri akinamama waanzishe event ya kuwafundisha akimama wenzao jinsi ya kuogelea na kujiokoa na majanga ya maji "mara nyingi kati ya ajali mbaya zinazotokea za mafuriko, kuzama kwa meli nk. waathirika wakubwa ni akinamama na watoto pia amewashukuru akinamama waliokubali kuunda kamati hiyo na kuwasaidia wananwake wenzao, na ametoa wito kwa wafadhili mbalimbali, taasisi, makampuni na watu binafsi kujitolea kuwezesha na kufanikisha event ya Mv Mama.
katika kuhakikisha event hii inafanikiwa vilivyo mama SS Omar (mshauri mkuu) amewataka akina baba wawaruhusu akinamama hao kushiriki katika event ya Mv mama bila vipingamizi.

Kwa upande wake Bi. Beatrice Mkunde ( Mhadhiri wa chuo cha Mwalimu Nyerere) ambaye ni katibu wa kamati hiyo alisema kamati ya akinamama hao imejipanga kikamilifu kuhakikisha event ya Mv Mama inafanikiwa kwa mafanikio makubwa. Event ya Mv Mama inatarajiwa kufanyika mwezi wa tano mwaka 2013 huko kigamboni.

Akifafanua zaidi mkufunzi mkuu  atakayeendesha event ya Mv Mama Bw. Geofrey Kimimba Mwakabende toka klabu ya Tanzania Marine Swimming alisema kuwa Mv Mama imetokana na jina la Meli ambayo inatumia nafsi ya kike kwa maana ya kwamba Meli sawa na mama kiusafi, uwezo wa ubebaji na  utendaji kazi kwa ujumla. Hivyo MV Mama itakuwa ni ujuzi ambao anaenda kupatiwa mwanamke kwa event hii ya kwanza lakini kwakutambua kuwa ukimuelimisha mwanamke umeelimisha jamii au ulimwengu mzima hivyo itaendelea kuwaelimisha hata wanaume na watu wa rika na jinsia zote kwa event zitakazofuata chini ya MV mama.
Mkufunzi huyo alisema kuwa kwa uzoefu wa klabu yake  watu ambao wamekuwa wakijitokeza kwa wingi  kwenye event mbalimbali walizowahi kuandaa ni wanaume zaidi kutokana na sababu za kihistoria, na kiutamaduni  ambapo wanawake wamekuwa wakipewa kazi za kwenda porini kuokota kuni ilihali wanaume wakifanya kazi za kuogelea na hatimae kuwa wavuvi na hivyo kupelekea kuwa mwanamke u binti wakitanzania akionekana kama ni mhuni au mtu anepotoka kimaadili pale anapoonekana akiogelea, licha ya mabadiliko tulionayo hivi sasa ambapo mwanamke ndiye anayewajibika mara nyingi na watoto pale anapokuwa anaenda nao  beach, kuchota maji mtoni, na kuwavusha mto.  Pia wanawake na watoto ndio waathirika wakubwa  wa mafuriko,na ajali za majini ambazo zimewahi kutokea hapa Tanzania.
Kwa mujibu wa mkufunzi mkuu wa klabu ya Tanzania Marine Swimming katika event ya MV Mama mambo yatakayofundishwa ni pamoja na;

  • Kanuni za usalama majini
  • Kuogelea
  • Jinsi ya kumuokoa mtu anaekufa maji
  • Jinsi ya kutoa msaada kwa aliyeokolewa kwenye  maji
  • Mbinu za kuvuka mito
  • Utumiaji wa vifaa vyakujiokolea
  • Jinsi ya kuihama meli
  • Jinsi yakusubiri msaada majini
  • Jinsi yakutunza mazingira ya maji na yale yanayozunguka vyanzo vya maji

Mwisho kabisa ni wito kwa wafadhili, watanzania, na watu  mbali mbali katika jamii kutambua umuhimu wa mafunzo haya na kujitoa kwa hali na mali kuweza kufanikisha  na kufanya mafunzo kama haya kuwa endelevu na kuweza kusaidia watanzania wengi  zaidi kunufaika nayo.

Marine Tanzania Swimming Club
+255 714 287 207
+255 788 343 051
+255 713 311 009
Tarehe 27 Machi 2013

Popular Posts